Showing 1-20 of 78 items.

Arrah"man, Mwingi wa Rehema

Amefundisha Qur"ani.

Amemuumba mwanaadamu,

Akamfundisha kubaini.

Jua na mwezi huenda kwa hisabu.

Na mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.

Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani,

Ili msidhulumu katika mizani.

Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.

Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.

Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.

Na nafaka zenye makapi, na rehani.

Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha

Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..

Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.

Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha

Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.

Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?

Anaziendesha bahari mbili zikutane;

Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.