Showing 1-20 of 62 items.

Naapa kwa nyota inapo tua,

Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.

Wala hatamki kwa matamanio.

Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa;

Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu,

Mwenye kutua, akatulia,

Naye yuko juu kabisa upeo wa macho.

Kisha akakaribia na akateremka.

Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.

Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia.

Moyo haukusema uwongo uliyo yaona.

Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona?

Na akamwona mara nyingine,

Penye Mkunazi wa mwisho.

Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa.

Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika.

Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.

Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola wake Mlezi.

Je! Mmemuona Lata na Uzza?

Na Manaat, mwingine wa tatu?