Showing 1-20 of 55 items.

Saa imekaribia, na mwezi umepasuka!

Na wakiona Ishara hugeuka upande na husema: Huu uchawi tu unazidi kuendelea.

Na wamekanusha na wamefuata matamanio yao. Na kila jambo ni lenye kuthibiti.

Na bila ya shaka zimewajia khabari zenye makaripio.

Hikima kaamili; lakini maonyo hayafai kitu!

Basi jiepushe nao. Siku atakapo ita mwitaji kuliendea jambo linalo chusha;

Macho yao yatainama; watatoka makaburini kama nzige walio tawanyika,

Wanamkimbilia mwitaji, na makafiri wanasema: Hii ni siku ngumu.

Kabla yao kaumu ya Nuhu walikanusha; wakamkanusha mja wetu, na wakasema ni mwendawazimu, na akakaripiwa.

Basi akamwomba Mola wake Mlezi akasema: Kwa hakika mimi nimeshindwa, basi ninusuru!

Basi tukaifungua milango ya mbingu kwa maji yanayo miminika.

Na tukazipasua ardhi kwa chemchem, yakakutana maji kwa jambo lilio kadiriwa.

Na tukamchukua kwenye safina ya mbao na kamba.

Ikawa inakwenda kwa nadhari yetu, kuwa ni malipo kwa alivyo kuwa amekanushwa.

Na bila ya shaka tuliiacha iwe ni Ishara. Lakini je, yupo anaye kumbuka?

Basi ilikuwaje adhabu yangu, na maonyo yangu.

Na bila ya shaka Sisi tumeifanya Qur"ani iwe nyepesi kufahamika. Lakini yupo anaye kumbuka?

Kina A"di walikanusha. Basi ilikuwaje adhabu yangu na maonyo yangu?

Hakika Sisi tuliwapelekea upepo wa kimbunga katika siku korofi mfululizo,

Ukiwang"oa watu kama vigogo vya mitende vilio ng"olewa.